Mark 12:36 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Daudi mwenyewe, akinena kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, alisema: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Daudi mwenyewe kwa kupitia Roho Mtakatifu alisema, ‘Bwana Mungu alimwambia Bwana Mfalme wangu: Keti karibu nami upande wangu wa kuume, nami nitawaweka adui zako chini ya udhibiti wako.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, Mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Daudi mwenyewe akinena kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu alisema: “ ‘BWANA alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Daudi mwenyewe, akinena kwa kuongozwa na Roho wa Mwenyezi Mungu, alisema: “ ‘ bwana Mwenyezi alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi mwenyewe alisema kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu, mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi yeye mwenyewe, akiongozwa na Roho Mutakatifu, alisema: ‘Bwana wetu Mungu alimwambia Bwana wangu: Ikaa na mamlaka kwa kuume kwangu, mpaka nitakapoweka waadui zako chini ya miguu yako.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu Daud mwenyewe alisema, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume Hatta niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako.