Mark 12:37 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanawe?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?” Umati ule wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Daudi anamwita Masihi ‘Bwana’. Itakuwaje tena Kristo awe yote Bwana na pia mwana wa Daudi?” Hapo lilikuwepo kundi kubwa la watu liliokuwa likimsikiliza kwa furaha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanae?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanawe?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?” Ule umati wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?” Ule umati wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na watu wengi walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanawe?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Dawidi mwenyewe akimwita Bwana, anakuwaje tena mwana wake? Kwa kuwa watu wengi walipendezwa kumsikiliza,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi mwenyewe anamwita Kristo ‘Bwana’; namna gani basi Kristo anaweza kuwa Mwana wake?” Kundi kubwa la watu walimusikiliza Yesu kwa furaha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Daud mwenyewe amwita Bwana: bassi amekuwaje mwana wake? Na ule mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.