Mark 12:38 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa akifundisha, Isa alisema, “Jihadharini na walimu wa Torati. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia katika mafundisho yake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika mafundisho yake alisema, “Jihadharini na walimu wa Sheria.” Wao wanapenda kutembea huko na huko katika mavazi yanayopendeza huku wakipenda kusalimiwa masokoni,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokuwa akifundisha, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu na kusalimiwa kwa heshima masokoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa akifundisha, Isa alisema, “Jihadharini na walimu wa Torati. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia katika mafundisho yake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema na kuwafundisha: Jiangalieni kwa ajili ya waandishi wanaotaka kutembea wenye kanzu ndefu na kuamkiwa na watu sokoni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia katika mafundisho yake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mafundisho yake aliwaambia: “Mujiepushe na walimu wa Sheria, wanaopenda kujitembeza wakivaa kanzu ndefu, na kusalimiwa kwa heshima kwenye nafasi ya makutano.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia katika mafundisho yake, Jibadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni,