Mark 12:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akamtuma tena mtumishi mwingine; huyu pia wakamwumiza kichwa na kumtendea vibaya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha yule mwenye shamba akamtuma mtumishi mwingine kwao; nao wale wakulima wakampiga kichwani na kumfanyia mambo ya aibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia jeraha za kichwa, wakamfanyia jeuri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akamtuma mtumishi mwingine kwao. Huyu naye wakampiga kichwani na kumtendea mambo ya aibu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akatuma tena mtumishi mwingine; huyu wakamuumiza kichwa na kumtendea vibaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akamtuma tena mtumishi mwingine; huyu pia wakamwumiza kichwa na kumtendea vibaya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha yule mwenye shamba akamtuma mtumishi mwingine kwao, wale wakulima wakampiga kichwani na kumfanyia mambo ya aibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha yule mwenye shamba akamtuma mtumishi mwingine kwao; nao wale wakulima wakampiga kichwani na kumfanyia mambo ya aibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia majeraha ya kichwa, wakamfanyia jeuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akamtuma tena mtumishi mwingine; huyu pia wakamwumiza kichwa na kumtendea vibaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, naye wakampiga na kumtia vidonda vya kichwani na kumtukana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia jeraha za kichwa, wakamfanyia jeuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwenye shamba akatuma tena kwao mutumishi mwingine. Yule naye, wakamwumiza kwenye kichwa na kumutukana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na huyo wakampiga mawe, wakamtia jeraha ya kichwa, wakamtoa ametiwa aibu.