Mark 12:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huwadhulumu wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu! Siku ya hukumu watapata adhabu kali.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambao hula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu; hawa watapata hukumu iliyo kubwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hawa huwadanganya wajane ili wazichukue nyumba zao na wanasali sala ndefu ili kujionesha kwa watu. Watu hawa watapata hukumu iliyo kubwa zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huwanyonya wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu. Siku ya hukumu watapata adhabu kali!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huwadhulumu wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu! Siku ya hukumu watapata adhabu kali.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao hula nyumba za wajane na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Watapata adhabu iliyo kuu sana.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambao hula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu; hawa watapata hukumu iliyo kubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huwadhulumu wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu! Siku ya hukumu watapata adhabu kali.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huzila nyumba za wajane wakijitendekeza, kama wanakaza kuwaombea. Walio hivyo mapatilizo yao yatakuwa kuliko ya wengine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambao hula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu; hawa watapata hukumu iliyo kubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wananyanganya mali ya wajane na kuomba maombi marefu kusudi waonekane mbele ya watu. Kwa sababu hii watahukumiwa vikali sana!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu: hawa watapokea hukumu iliyo kubwa.