Mark 12:44 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana wengine wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali yao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake, akaweka kila kitu alichokuwa nacho, hata kile alichohitaji ili kuishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa kuwa wote walitoa kile cha ziada walichokuwa nacho. Lakini yeye katika umasikini wake, aliweka yote aliyokuwa nayo. Na hiyo ilikuwa fedha yote aliyokuwa nayo kutumia wa maisha yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana wengine wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mjane kutokana na umaskini wake, ametoa kila kitu alichokuwa nacho, hata kile alichohitaji ili kuishi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake, akaweka kila kitu alichokuwa nacho, hata kile alichohitaji ili kuishi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana wengine wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wote walitoa mali katika mali zao nyingi, lakini huyu kwa ukiwa wake amevitoa vyote, alivyokuwa navyo, ndivyo vyote vilivyomlisha.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana wengine wote walitoa sehemu ya mali wasiyokuwa nayo lazima. Lakini yeye ametoa kwa umasikini wake, mali yote aliyokuwa nayo kwa kuishi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
maana hawa wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi: bali huyu katika mahitaji yake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndio maisha yake yote pia.
Recommended Reading