Mark 12:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpenzi. Mwishowe akamtuma huyo akisema, ‘Watamjali mwanangu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwenye shamba alikuwa bado na mmoja wa kumtuma, mwanawe aliyempenda. Hatimaye akamtuma akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hata hivyo mwenye shamba yule bado alikuwa na mmoja wa kumtuma, mwanaye mpendwa. Alimtuma akiwa mtu wa mwisho. Akasema, ‘nina hakika watamheshimu mwanangu!’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpendwa. Mwishowe akamtuma huyo akisema, Watamheshimu mwanangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpenzi. Mwishowe akamtuma huyo akisema, ‘Watamjali mwanangu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwenye shamba alikuwa amebakiwa na mmoja wa kumtuma, huyu ni mwanawe mpendwa. Hatimaye akamtuma akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwenye shamba alikuwa bado na mmoja wa kumtuma, mwanawe aliyempenda. Hatimaye akamtuma akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpenzi. Mwishowe akamtuma huyo akisema, ‘Watamjali mwanangu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alikuwa na mmoja tena, ndiye mwanawe mpendwa; huyo akamtuma kwao wa mwisho akisema: Watamcha mwanangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwenye shamba alibaki tu na mutu mumoja, naye alikuwa mwana wake mupendwa. Mwisho akamutuma kwao, akisema: ‘Ninajua kwamba watamuheshimu mwana wangu.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi alikuwa na mwana mmoja bado, mpendwa wake; huyu nae akamtuma kwao wa mwisho, akinena, Watamjali mwana wangu.