Mark 13:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alipokuwa anatoka hekaluni mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipokuwa akitoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu! Tazama jinsi mawe haya yalivyo makubwa, na majengo haya yalivyo mazuri!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alikuwa akiondoka katika eneo la Hekalu na moja ya wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu, tazama mawe haya yanavyopendeza na jinsi majengo haya yanavyopendeza!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alipokuwa anatoka hekaluni mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Yesu alipokuwa akitoka Hekaluni, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu! Tazama jinsi mawe haya yalivyo makubwa na majengo haya yalivyo mazuri!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipokuwa akitoka Hekaluni, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu! Tazama jinsi mawe haya yalivyo makubwa, na majengo haya yalivyo mazuri!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alipokuwa anatoka hekaluni mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipotoka Patakatifu, mwanafunzi wake mmoja akamwambia: Mfunzi, yatazame mawe hayo makubwa na majengo hayo makubwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipokuwa akitoka katika hekalu, mumoja kati ya wanafunzi wake akamwambia: “Mwalimu, angalia mawe haya mazuri na majengo haya makubwa!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
HATTA alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, Mwalimu, namna gani ya mawe! namna gani ya majengo!