Mark 13:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si nyinyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke awali kuhusu mtakalosema. Semeni tu lolote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho Mtakatifu wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati wowote watakapowakamata na kuwashitaki, msiwe na wasiwasi kujiandaa kwa yale mtakayoyasema, lakini myaseme yale mtakayopewa saa ile ile, kwa kuwa si ninyi mnaozungumza; bali, ni Roho Mtakatifu anayezungumza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si nyinyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke kuhusu mtakalosema. Semeni tu lo lote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi msemao bali ni Roho Mtakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke awali kuhusu mtakalosema. Semeni tu lolote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lolote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si nyinyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo, watakapowatoa na kuwapeleka, msianze kuyahangaikia maneno ya kusema, ila maneno mtakayopewa saa ile yasemeni yaleyale! Kwani si ninyi mnaosema, ila ni Roho Mtakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mutakapokamatwa na kupelekwa kwa kuhukumiwa, musijihangaishe mbele ya wakati juu ya maneno mutakayosema, lakini museme maneno mutakayopewa saa ile ile. Kwa sababu hayatatoka kwenu wenyewe, lakini yatatoka kwa Roho Mutakatifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na watakapowachukueni, na kuwateni katika mikono ya watu, msianze kuwaza mtakayosema, wala msishughulike: lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni: kwa maana si ninyi mseniao, hali Roho Mtakatifu.