Mark 13:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtakapoona ‘Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake), hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtakapoona ‘chukizo la uharibifu’ limesimama mahali pasipolipasa (asomaye na afahamu), basi wale walio Yudea wakimbilie milimani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati mtakapoliona chukizo la uharibifu likisimama mahali pasipotakiwa lisimame.” (Msomaji aelewe hii ina maana gani?) “Kisha wale waliopo katika Uyahudi wakimbilie milimani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mtakapoona Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtakapoona ‘Chukizo Haribifu’ limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake), hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mtakapoona chukizo la uharibifu limesimama mahali pasipolipasa (asomaye na afahamu), basi wale walioko Uyahudi na wakimbilie milimani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mtakapoona ‘chukizo la uharibifu’ limesimama mahali pasipolipasa (asomaye na afahamu), basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Yudea na wakimbilie milimani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtakapoona ‘Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake), hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, mtakapochafukwa mioyo mkiona, mwangamizaji atapishaye akisimama mahali pasipompasa; mwenye kupasoma hapa sharti aangalie, ajue maana! Siku zile watakaokuwako Yudea na wakimbilie milimani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini mutamwona yule anayeitwa ‘Chukizo Linaloleta Uharibifu,’ akisimamishwa pahali asipopaswa kuwa. (Anayesoma maneno haya aelewe maana yake). Basi watakaokuwa Yudea, wakimbilie kwa milima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu (lile lililoneuwa ua nabii Danieli) likisimama pasipolipasa (asomae na afahamu) ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani;