Mark 13:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama Bwana asingepunguza siku hizo hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kama Mwenyezi Mungu hangefupisha siku hizo, kamwe hakuna mtu yeyote angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, wale aliowachagua, amezifupisha siku hizo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama Bwana asingelifupisha muda huo, hakuna ambaye angenusurika. Lakini yeye amefupisha siku hizo kwa ajili ya watu wale aliowateuwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama Bwana asingepunguza siku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama Bwana asingepunguza siku hizo hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama Bwana asingelifupiza siku hizo, kamwe asingeliokoka mtu ye yote, lakini kwa ajili ya wateule, wale aliowachagua, amezifupiza siku hizo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama Mwenyezi Mungu asingelifupisha siku hizo, kamwe asingeliokoka mtu yeyote. Lakini kwa ajili ya wateule, wale aliowachagua, amezifupisha siku hizo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama Bwana asingepunguza siku hizo hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo siku zile kama Bwana hangalizipunguza, hangaliokoka mtu hata mmoja. Lakini kwa ajili ya wale, waliochaguliwa, aliowachagua, amezipunguza siku zile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama Bwana asingepunguza siku zile za mateso, hakuna hata mutu mumoja ambaye angeponyoka kufa. Lakini kwa ajili ya wachaguliwa aliowachagua amezipunguza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kama Bwana asingalizikatiza siku zile, asingeokoka mtu aliye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku zile.