Mark 13:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Jifunzeni somo hili kutoka katika mti wa mtini: Matawi yake yanaponyauka na kubeba majani, unajua kwamba kiangazi kimekaribia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Mara mwonapo matawi yake yakichipua na kutoa majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jifundisheni mfano kwa mkuyu: matawi yake yanapochipua na kuchanua majani, mnatambua, ya kuwa siku za vuli ziko karibu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Muangalilie mufano juu ya muti wa tini. Wakati matawi yake yanapochipuka, nayo majani yao yanapochipuka, ninyi munatambua kwamba wakati wa jua kali unakaribia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liauzapo kuwa laini, na kuchanua majani yake, mwajua ya kuwa karibu wakati wa bari: