Mark 13:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna anayejua wakiwemo malaika wa mbinguni ama Mwana bali baba peke yake lini siku au saa ile itakapowadia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini kwa habari ya siku ile na saa hakuna ye yote ajuaye, hata malaika walioko mbinguni wala Mwana hajui, ila Baba peke yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ile siku au saa yake itakapofikia, mtu hapajui, wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini hakuna mutu anayejua siku ile au saa, hata wamalaika wanaokuwa mbinguni, hata Mwana; isipokuwa Baba peke yake tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini khabari ya siku ile na saa ile hakuna aijuae, hatta malaika walio mbinguni, wala Mwana, illa Baba.