Mark 13:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia na mlinzi wa mlango awe macho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni kama mtu anayesafiri. Anaiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwamuru yule bawabu aliye mlangoni akeshe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni kama mtu anayeenda safarini na kabla ya kuondoka huiacha nyumba yake mikononi mwa watumishi wake. Kabla ya kuiacha nyumba yake anawaweka watumishi wake kusimamia kila mmoja akiwa na kazi yake maalumu. Kisha atamwamuru mlinzi mlangoni awe macho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia na mlinzi wa mlango awe macho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni kama mtu anayesafiri akiiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwambia yule bawabu aliye mlangoni akeshe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni kama mtu anayesafiri. Anaiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwamuru yule bawabu aliye mlangoni akeshe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia na mlinzi wa mlango awe macho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, hivyo kesheni! Kwani hamjui, mwenye nyumba atakaporudia, kama atakuja jioni au kati ya usiku au jogoo awikapo au mapema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Itakuwa kama vile mutu anayefunga safari. Alipotoka kwake akawaachia watumishi madaraka yake, akimupa kila mutu kazi yake. Vilevile akamwagiza mulinzi wa mulango akeshe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ni kana kwamba mtu mwenye kusafiri, ameacha nyumba yake, amewapa amri watumwa wake, na killa mtu kazi yake, amemwamuru bawabu akeshe.