Mark 13:35 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Vivyo hivyo ni lazima mjihadhari, kwa sababu hamjui ni muda gani mkuu wa nyumba atakuja; hamjui kama atakuja jioni, usiku wa manane, wakati jogoo anawika, au alfajiri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Basi kesheni kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi, iwapo ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au wakati wa mapambazuko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Basi kesheni kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jogoo, au asubuhi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asije na kuwastusha akiwakuta, mmelala.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi muangalie sababu hamujui wakati bwana wa nyumba atakaporudi: labda magaribi, au katikati ya usiku, au wakati jogoo anapowika, au asubui.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kesheni bassi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au usiku wa manane, au awikapo jogoo, an assubuhi: