Mark 13:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msikiapo habari za vita na uvumi wa vita, msiwe na hofu. Mambo haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtasikia juu ya vita vinavyopiganiwa na mtasikia habari juu ya vita vingine vinavyoanza. Hata hivyo msishtushwe. Mambo hayo lazima yatokee, kabla ule mwisho wenyewe kufika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msikiapo habari za vita na uvumi wa vita, msiwe na hofu. Mambo haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msikiapo habari za vita na uvumi wa vita, msiwe na hofu. Mambo haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nao watapoteza wengi. Nanyi mtakaposikia vita na mavumi ya vita msivihangaikie! Hivyo sharti viwepo, lakini huo sio mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutakaposikia habari za matokeo au utetezi wa vita musiogope. Sherti mambo hayo yatukie, lakini hayaonyeshi kama mwisho umefika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena mtakaposikia vita na khabari za vita, msitishwe: maana hayana buddi kutukia, lakini mwisho wenyewe bado.