Mark 14:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya mikate isiyotiwa chachu. Makuhani wakuu na waalimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila, wamuue.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka, na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Isa kwa hila na kumuua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilikuwa yapata siku mbili kabla ya Sikukuu ya Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Wakuu wa makuhani na walimu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia, kwa ujanja fulani, ya kumkamata na kumuua Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya mikate isiyotiwa chachu. Makuhani wakuu na waalimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila, wamuue.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Yesu kwa hila na kumwua,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka, na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Isa kwa hila na kumuua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya mikate isiyotiwa chachu. Makuhani wakuu na waalimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila, wamuue.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Palikuwa pamesalia siku mbili kuwa sikukuu ya Pasaka na ya mikate isiyotiwa chachu. Nao watambikaji wakuu na waandishi wakatafuta kumkamata kwa werevu, wapate kumwua;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa kumebaki siku mbili mbele ya kutimia kwa sikukuu ya Pasaka na ya Mukate Usiyotiwa Chachu. Wakubwa wa makuhani na walimu wa Sheria walitafuta njia ya kumukamata Yesu kwa werevu kusudi wamwue.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BAADA ya siku mbili ilikuwa siku kuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa: makuhani wakuu na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.