Mark 14:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, alikwenda kwa makuhani wakuu ili kumsaliti Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa viongozi wa makuhani ili kumsaliti Isa kwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yuda Iskariote, yule mmoja katika wale Thenashara, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na mbili, aliwaendea viongozi wa makuhani ili kumsaliti Yesu kwao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, alienda kwa makuhani wakuu ili kumsaliti Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, alikwenda kwa makuhani wakuu ili kumsaliti Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili wa Bwana Yesu, akaenda kwa viongozi wa makuhani ili kumsaliti Yesu kwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa viongozi wa makuhani ili kumsaliti Isa kwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yuda Iskarioti, yule mmoja katika wale Kumi na Wawili, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, alikwenda kwa makuhani wakuu ili kumsaliti Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yuda Iskariota aliyekuwa mwenzao wale kumi na wawili akaenda zake kwa watambikaji wakuu, amtie mikononi mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yuda Iskariote, yule mmoja katika wale Thenashara, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yuda Iskariota, mumoja wa wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa wakubwa wa makuhani, kusudi amutoe Yesu kwao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yuda Iskariote, mmoja wa wathenashara, akaenda zake kwa makuhani wakuu, apate kumsaliti kwao.