Mark 14:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya kwanza ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wakati ambapo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile pasaka?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, ambapo kila mara mwana kondoo alitolewa sadaka kwa ajili ya Pasaka. Wanafunzi wa Yesu wakamwendea na kumwuliza, “Ni wapi unapotaka tuende kukuandalia ili uweze kuila Karamu ya Pasaka?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wakati ambapo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya kwanza ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wakati ambapo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Yesu wakamwuliza, “Unataka tuende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile Pasaka?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya kwanza ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wakati ambapo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya kwanza ya kula mikate isiyotiwa chachu, watu walipochinjia kondoo ya Pasaka, wanafunzi wake wakamwuliza: Unataka, twende, tukuandalie wapi, uile kondoo ya Pasaka?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile pasaka?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya kwanza ya karamu ya sikukuu ya Mukate Usiyotiwa Chachu, wakati ambapo walichinja kondoo wa Pasaka, wanafunzi wa Yesu wakamwuliza: “Unataka tuende wapi kukutayarishia karamu ya Pasaka?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Wapi unataka tuende tukaandalie uile pasaka?