Mark 14:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye atawaonesha chumba kikubwa ghorofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalieni humo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atawaonesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye atawaonesha chumba kikubwa ghorofani, klichoandaliwa tayari kwa ajili yetu. Basi mtuandalie chakula pale.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalieni humo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye atawaonesha chumba kikubwa ghorofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalieni humo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mwenyewe atawaonesha ghorofa kubwa, iliyotayarishwa; humo tuandalieni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye atawaonesha chumba kikubwa ghorofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalieni humo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mwenyewe atakapowaonyesha chumba kikubwa kilichokwisha kutandikwa; namo mle tuandalieni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye atawaonyesha chumba kikubwa cha gorofi, kilichokwisha kupangwa vizuri na kuwa tayari. Ni mule mutakapotutayarishia karamu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae mwenyewe atawaonyesha orofa kuhwa, imetandikwa tayari: huko tuandalieni.