Mark 14:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula, mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya nardo safi ya thamani kubwa alikuja, akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu marashi hayo kichwani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma. Alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alikuwa Bethania, katika nyumba ya Simoni mwenye ugonjwa mbaya sana wa ngozi. Wakati ameketi mezani mwanamke mmoja alimwijia. Naye alikuwa na gudulia la mawe lililojaa manukato ya bei ghali yaliyotengenezwa kwa nardo safi. Mwanamke huyo alilifungua gudulia lile kwa kulivunja na kumwagia Yesu manukato kichwani mwake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula, mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya nardo safi ya thamani kubwa alikuja, akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu marashi hayo kichwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula, mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya nardo safi ya thamani kubwa alikuja, akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu marashi hayo kichwani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alipokuwa huko Bethania nyumbani kwa Simoni aliyekuwa na ukoma, wakati alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni aliyekuwa na ukoma. Wakati alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mwenye ukoma, akiwa amekaa mezani, alikuja mwanamke mwenye chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa; akaivunja chupa akaimimina kichwani pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula, mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya nardo safi ya thamani kubwa alikuja, akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu marashi hayo kichwani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipokuwa Betania nyumbani mwa Simoni Mkoma akikaa chakulani, akamjia mwanamke mwenye kichupa chepe cha jiwe kilichojaa mafuta ya maua yanayoitwa Narada; ni yenye bei kubwa, nayo yalikuwa hayakuchanganywa na mengine. Akakivunja kile kichupa, akayamiminia kichwani pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alikuwa Betania katika nyumba ya mutu aliyeitwa Simoni Mukoma. Walipokuwa wakikula, mwanamuke mumoja akaingia ndani ya nyumba. Alikuwa na chupa la jiwe lenye marasi ya bei kali yaliyotengenezwa na maua ya nardo safi. Kisha akavunja mudomo wa lile chupa na kumimia marasi juu ya kichwa cha Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae akiwapo Bethania, nyumbani mwa Simon mwenye ukoma, ameketi chakulani, akaja mwanamke mwenye kibweta cha alabastro cha marhamu ya hali udi, safi, ya thamani nyingi; akakivunja kibweta cha alabastro akaimimina kichwani pake.