Mark 14:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo Yesu akamjibu kusema, “Ukweli ni kwamba, usiku wa leo utasema kuwa hunijui. Utasema hivyo mara tatu kabla ya jogoo kuwika mara mbili.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamwambia, “Kweli nakwambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akamwambia: Kweli nakuambia: Usiku huu wa leo jogoo atakapokuwa hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamujibu: “Kweli ninakuambia kwamba usiku huu, mbele jogoo hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, Wewe leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo marra mbili, utanikana marra tatu.