Mark 14:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi ya watu waliokuwa hapo walikasirika, wakajisemea, “Kwa nini kupoteza ovyo marashi haya?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadhi ya watu waliokuwa pale walikasirika na wakasemezana, “Upotevu huu wote wa manukato ni wa nini?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya watu waliokuwa pale walikasirika na kulalamika miongoni mwao, “Kwa nini kuwepo na ufujaji wa manukato namna hii?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadhi ya watu waliokuwa hapo walikasirika wakajisemea, “Kwa nini kupoteza ovyo marashi haya?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi ya watu waliokuwa hapo walikasirika, wakajisemea, “Kwa nini kupoteza ovyo marashi haya?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya watu waliokuwapo pale walikuwa wakisemezana wao kwa wao, “Kwa nini ubadhirifu huu wa manukato?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya watu waliokuwepo pale walikuwa wakisemezana wao kwa wao, “Upotevu huu wote ni wa nini?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwa nini kupoteza marhamu namna hii?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi ya watu waliokuwa hapo walikasirika, wakajisemea, “Kwa nini kupoteza ovyo marashi haya?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mlikuwamo waliochukiwa mioyoni mwao kwamba: Upotevu huu wa haya mafuta mazuri sana ni wa nini?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wamoja kati ya watu waliokuwa pale wakachukizwa na kitendo kile na kusemezana: “Kwa nini kupoteza mali namna hii?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Palikuwa na watu waliochukiwa katika nafsi zao wakisema, Ya nini kupoteza marhamu namna hii?