Mark 14:41 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipowajia mara ya tatu aliwaambia, “Mnalala bado na kupumzika? Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana wa Mtu anakabidhiwa kwa watu waovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazameni, Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaja mara ya tatu, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike; yatosha, saa imekuja; tazama, Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alirudi mara ya tatu na kuwaambia, “Je, bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imefika. Mwana wa Adamu atasalitiwa mikononi mwa watenda dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipowajia mara ya tatu aliwaambia, “Mnalala bado na kupumzika? Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana wa Mtu anakabidhiwa kwa watu waovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipowajia mara ya tatu aliwaambia, “Mnalala bado na kupumzika? Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana wa Mtu anakabidhiwa kwa watu waovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazama, Mwana wa Adamu anasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazameni, Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaja mara ya tatu, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike; yatosha, saa imekuja; tazama, Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipowajia mara ya tatu aliwaambia, “Mnalala bado na kupumzika? Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana wa Mtu anakabidhiwa kwa watu waovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokuja mara ya tatu akawaambia: Mwafuliza kulala usingizi, uchovu uwatoke? Pametimia, saa imefika; tazameni, Mwana wa mtu anatiwa mikononi mwa wakosaji!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaja mara ya tatu, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike; yatosha, saa imekuja; tazama, Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliporudi kwa mara ya tatu, akawaambia: “Mungali munalala na kupumzika? Inatosha! Saa imetimia. Sasa Mwana wa Mutu anatolewa katika mikono ya wenye zambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaja marra ya tatu, akawaambia, Laleni sasa, hatta mwisho, kapumzikeni: yatosha, saa imekuja; Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi.