Mark 14:47 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesu, akachomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu aliuchomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mmoja wao waliokuwapo akafuta upanga, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mmoja wa wale waliosimama naye karibu akautoa upanga wake alani, akampiga nao mtumishi wa kuhani mkuu na kulikata sikio lake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesu akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesu, akachomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu akachomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu aliuchomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mmoja wao waliokuwapo akafuta upanga, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesu, akachomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mmoja wao waliosimama hapo akauchomoa upanga wake, akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mmoja wao waliokuwapo akafuta upanga, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mumoja kati ya wale waliokuwa pale, akachomoa upanga wake na kumukata mutumishi wa Kuhani Mukubwa sikio.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mmoja wao waliohudhuria akavuta upanga, akampiga mtumwa wa kuhani mkuu, akamkata sikio.