Mark 14:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi cha dinari 300, wakapewa maskini!” Wakamkemea huyo mama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Manukato haya yangeuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung'unikia sana yule mwanamke.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Gharama yake ni sawa na mshahara wa mwaka mzima. Manukato haya yangeweza kuuzwa na fedha hiyo kupewa walio maskini.” Kisha wakamkosoa yule mwanamke kwa hasira kwa jambo alilolifanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi cha denari mia tatu, wakapewa maskini!” Wakamkemea huyo mama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi cha dinari 300, wakapewa maskini!” Wakamkemea huyo mama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mafuta haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari 300 na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mafuta haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari 300, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung'unikia sana yule mwanamke.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi cha dinari 300, wakapewa maskini!” Wakamkemea huyo mama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mafuta haya yangaliwezekana kuuzwa kwa shilingi 300 na kupita, wakapewa maskini! Kwa hiyo wakamfokea sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung’unikia sana yule mwanamke.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Marasi hii ingeweza kuuzishwa kwa bei ya vikoroti mia tatu vya feza na kugawanyia wamasikini mali ile.” Na wakamukasirikia yule mwanamuke vikali.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
maana marhamu hii ingalikuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi wakapewa maskini. Wakamnungʼunikia sana yule mwanamke.