Mark 14:54 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro alimfuata Yesu kwa mbali, akaingia ndani ya ua wa kuhani mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Petro akamfuata kwa mbali, hata ndani katika behewa ya Kuhani Mkuu; akawa ameketi pamoja na watumishi, anakota moto mwangani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akamfuata Yesu kwa mbali kidogo hadi ndani ya baraza la nyumba ya kuhani mkuu. Petro alikuwa ameketi na wale walinzi akijipasha joto na moto walioukoka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro alimfuata Yesu kwa mbali, akaingia ndani ya ya wa Kuhani Mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro alimfuata Yesu kwa mbali, akaingia ndani ya ua wa kuhani mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro akamfuata kwa mbali, mpaka kwenye ua wa Kuhani Mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Petro akamfuata kwa mbali, hadi ndani katika behewa ya Kuhani Mkuu; akawa ameketi pamoja na watumishi, akiota moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro alimfuata Yesu kwa mbali, akaingia ndani ya ua wa kuhani mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Petero akamfuata mbalimbali, mpaka akaingia uani kwa mtambikaji mkuu, akakaa pamoja na watumishi penye mwangaza akiota moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Petro akamfuata kwa mbali, hata ndani katika behewa ya Kuhani Mkuu; akawa ameketi pamoja na watumishi, anakota moto mwangani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Petro akamufuata Yesu kwa mbali, hata akaingia ndani ya upango wa nyumba ya Kuhani Mukubwa. Pale akaikaa pamoja na walinzi, akiota moto.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Petro akamfuata mbali, hatta ndani katika behewa ya kuhani mkuu; akaketi pamoja na watumishi, anakota moto.