Mark 14:55 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu wapate kumwua, lakini hawakuupata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Isa ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua; wasione.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Viongozi wa makuhani na Baraza lote la Wayahudi walikuwa wakitafuta ushahidi dhidi ya Yesu wa kuweza kumhukumu kifo, lakini hawakupata kitu chochote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu wapate kumwua, lakini hawakupata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu wapate kumwua, lakini hawakuupata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Viongozi wa makuhani na wajumbe wote wa Baraza walikuwa wanatafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumwua, lakini hawakupata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Isa ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua; wasione.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu wapate kumwua, lakini hawakuupata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watambikaji wakuu na baraza ya wakuu wote wakamtafutia Yesu ushuhuda, wapate kumwua, lakini hawakuupata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua; wasione.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wa makuhani na wakubwa wote wa Baraza Kubwa walitafuta mashitaki juu ya Yesu kusudi wapate kumwua, lakini hawakupata neno.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Makuhani wakuu na baraza wote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua: wasione.