Mark 14:60 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kuhani mkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Isa, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Kuhani Mkuu akasimama katikati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha kuhani mkuu akasimama mbele yao na akamwuliza Yesu, “Je, wewe hutajibu? Nini ushahidi huu ambao watu wanaleta dhidi yako?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Kuhani Mkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kuhani mkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani Mkuu akasimama mbele ya hilo Baraza akamwuliza Yesu, “Je, wewe huwezi kujibu mashtaka haya ambayo watu hawa wameleta juu yako?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Isa, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Kuhani Mkuu akasimama katikati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kuhani mkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtambikaji mkuu alipoinuka, akaja katikati, akamwuliza Yesu akisema: Hujibu neno, hawa wanayokusimangia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Kuhani Mkuu akasimama katikati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Kuhani Mukubwa akasimama katikati ya watu na kumwuliza Yesu: “Haujibu hata neno? Watu hawa wanakushitakia nini?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kuhani mkuu akasimama kati kati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wakushuhudiani?