Mark 14:65 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, baadhi yao wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, wakampiga na kumwambia, “Bashiri ni nani amekupiga!” Hata watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakampiga makofi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na wengine walianza kutema mate, na kufunika uso wake, na kumpiga, na kumwambia, “Uwe nabii na utuambie nani aliyekupiga.” Kisha wale walinzi walimchukua na kuendelea kumpiga.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, baadhi yao wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, wakampiga na kumwambia, “Bashiri ni nani aliyekupiga!” Hata watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, baadhi yao wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, wakampiga na kumwambia, “Bashiri ni nani amekupiga!” Hata watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate, wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri ni nani aliyekupiga!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakamchukua wakampiga makofi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, baadhi yao wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, wakampiga na kumwambia, “Bashiri ni nani amekupiga!” Hata watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wengine wakaanza kumtemea mate, tena wakamfunika uso, wakampiga makonde, wakamwambia: Fumbua! Nao watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakampiga makofi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wengine katikati yao wakaanza kumutemea Yesu mate, wakamufunika uso na kumupiga ngumi, wakimwambia: “Tambua sasa ni nani aliyekupiga!” Nao waaskari walinzi wakamukamata Yesu na kumupiga makofi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wengine wakaanza kumtemea mate, na kumfunika uso, na kumpiga konde, na kumwambia, Fanya unabii. Watumishi wakampiga makofi.