Mark 14:72 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo jogoo akawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbuka jinsi Yesu alivyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Petro akabubujika machozi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Isa alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mara jogoo akawika mara ya pili. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mara jogoo akawika kwa mara ya pili, na Petro akakumbuka lile neno la Yesu alilomwambia: “Kabla kogoo hajawika mara ya pili utanikana mara tatu.” Naye akavunjika moyo na kuanza kulia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo jogoo akawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbuka jinsi Yesu alivyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Petro akabubujika machozi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo jogoo akawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbuka jinsi Yesu alivyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Petro akabubujika machozi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alilokuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Isa alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mara jogoo akawika mara ya pili. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo jogoo akawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbuka jinsi Yesu alivyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Petro akabubujika machozi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara hiyo jogoo akawika mara ya pili. Hapo Petero akalikumbuka lile neno, kama Yesu alivyomwambia: Jogoo atakapokuwa hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu. Alipovifikiri akaanza kulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mara jogoo akawika mara ya pili. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia. a.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara moja jogoo akawika kwa mara ya pili, na Petro akakumbuka maneno yale Yesu aliyomwambia kwamba mbele jogoo hajawika mara mbili, atakuwa amemukana mara tatu. Basi akaanza kulia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jogoo akawika marra ya pili. Petro akalikumbuka neno lile aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo marra mbili, utanikana marra tatu. Na alipolifikiri, akalia.