Mark 14:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni Habari Njema itakapohubiriwa, kitendo hiki alichofanya kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninawaambia kweli: Popote injili itakapohubiriwa ulimwenguni, kile alichokifanya kitasimuliwa kwa kumkumbuka.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni Habari Njema itakapohubiriwa, kitendo hiki alichofanya kitatajwa kwa ajili ya kumkumbuka.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni Habari Njema itakapohubiriwa, kitendo hiki alichofanya kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amin, amin nawaambia, mahali po pote duniani ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilotenda huyu mwanamke litatajwa kwa ukumbusho wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni Habari Njema itakapohubiriwa, kitendo hiki alichofanya kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli nawaambiani: Po pote katika ulimwengu wote, patakapotangazwa huu Utume mwema, patasemwa nacho hiki, alichokitenda yeye, naye akumbukwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kweli ninawaambia: kwa ajili ya kukumbuka mwanamuke huyu, tendo lile alilofanya litaelezwa popote Habari Njema itakapohubiriwa katika dunia nzima.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Amin, nawaamhieni, Killa ikhubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.