Mark 15:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, waalimu wa sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa Torati na Baraza la Wayahudi lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Isa, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Asubuhi na mapema, Mara tu ilipofika asubuhi viongozi wa makuhani, viongozi wazee wa Kiyahudi, walimu wa sheria, na baraza kuu lote la Wayahudi liliamua jambo la kufanya kwa Yesu. Walimfunga Yesu, wakamwondoa pale, na wakamkabidhi kwa Pilato.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, waalimu wa sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa Torati na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Isa, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, waalimu wa sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asubuhi kulipokucha, papo hapo watambikaji wakuu wakala njama pamoja na wazee na waandishi nao wote wa baraza ya wakuu wote, wakamfunga Yesu, wakampeleka, wakamtia mikononi mwa Pilato.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Asubui mapema, mara moja wakubwa wa makuhani wakafanya shauri pamoja na wasimamizi wa watu, walimu wa Sheria na wakubwa wote wa baraza. Wakamufunga Yesu, wakamupeleka na kwenda kumutoa kwa Pilato.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
MARRA ilipokuwa assubuhi makuhani wakuu wakafanya shauri pamoja na wazee na waandishi na haraza zima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta kwa Pilato.