Mark 15:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulubishe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi la rangi ya zambarau, wakamvika mavazi yake mwenyewe; wakamchukua nje ili wamsulibishe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walipomaliza kumkejeli walimvua joho lile la kizambarau, na kumvisha mavazi yake mwenyewe. Baada ya hapo wakamtoa nje ili waweze kumsulubisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika zile nguo zake mwenyewe. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulibishe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulubishe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi la rangi ya zambarau, wakamvika mavazi yake mwenyewe; wakampeleka nje ili wamsulubishe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha kumfyoza, wakamvua ile nguo nyekundu na kumvika nguo zake, wakampeleka nje, waje, wamwambe msalabani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi la rangi ya zambarau, wakamvika mavazi yake mwenyewe; wakamchukua nje ili wamsulibishe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokwisha kumuchekelea, wakamuvua ile nguo nyekundu na kumuvalisha nguo zake. Kisha wakaondoka naye inje kwa kwenda kumutundika juu ya musalaba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi jekundu, wakamvika nguo zake mwenyewe; wakamchukua nje wamsulibishe.