Mark 15:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha achukue msalaba wa Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Iskanda na Rufo, alikuwa anaingia mjini kutoka mashambani, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashamba, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakiwa njiani walikutana na mtu kutoka Kirenio aliyeitwa Simoni, akitoka vijijini kuja mjini. Yeye alikuwa baba yake Iskanda na Rufo. Wale wanajeshi wakamlazimisha kuubeba msalaba wa Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha achukue msalaba wa Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Aleksanda na Rufo, alikuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shamba, wakamlazimisha aubebe ule msalaba wa Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Iskanda na Rufo, alikuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shamba, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashambani, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha achukue msalaba wa Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakakamata mtu aliyepiga akitoka shambani; ni Simoni wa Kirene, baba yao Alekisandro na Rufu, wakamshurutisha, amchukulie msalaba wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashamba, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu mumoja wa Kurene, aliyeitwa Simoni, baba ya Alesanduro na Rufu, alikuwa akipita katika njia, akitoka kwenye vijiji. Waaskari wakamushurutisha abebe musalaba wa Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamtumikisha mtu aliyekuwa akipita, Simon Mkurene, akitoka mashamba, baba wa Iskander na Rufo, auchukue msalaba wake.