Mark 15:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao makuhani wakuu pamoja na waalimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani pamoja na walimu wa Torati wakamdhihaki miongoni mwao wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kadhalika na wakuu wa makuhani wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliponya wengine; hawezi kujiponya mwenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa njia hiyo hiyo, viongozi wa makuhani na walimu wa Sheria walimfanyia dhihaka na wakasema wao kwa wao, “Aliwaokoa wengine lakini hawezi kujiokoa mwenyewe!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nao makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao makuhani wakuu pamoja na waalimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo viongozi wa makuhani pamoja na walimu wa sheria wakamdhihaki miongoni mwao wakisema, “Yeye aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani pamoja na walimu wa Torati wakamdhihaki miongoni mwao wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kadhalika na wakuu wa makuhani wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliponya wengine; hawezi kujiponya mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao makuhani wakuu pamoja na waalimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vilevile nao watambikaji wakuu wakamfyoza pamoja na waandishi wakisema wao kwa wao: Wengine aliwaokoa, lakini mwenyewe hawezi kujiokoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kadhalika na wakuu wa makuhani wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliponya wengine; hawezi kujiponya mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile wakubwa wa makuhani na walimu wa Sheria kati yao walimusimanga Yesu, wakisemezana: “Aliokoa wengine, lakini sasa anashindwa kwa kujiokoa yeye mwenyewe!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kadhalika na makuhani wakuu wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliwaponya wengine; hawezi kujiponya nafsi yake.