Mark 15:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ati yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke kutoka msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi huyu Al-Masihi, huyu mfalme wa Israeli, ashuke sasa msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Hata wale waliosulibiwa pamoja naye wakamfyolea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa yeye kweli ni Masihi Mfalme wa Israeli, iinampasa ashuke sasa toka msalabani, tukiliona hilo nasi tutamwamini.” Wale wahalifu waliokuwa katika misalaba ile mingine pembeni waliosulubiwa pamoja naye nao walimtukana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ati yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke kutoka msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi huyu Kristo, huyu Mfalme wa Wayahudi, ashuke sasa kutoka msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulibiwa pamoja naye pia wakamtukana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi huyu Al-Masihi, huyu Mfalme wa Israeli, ashuke sasa kutoka msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Hata wale waliosulubiwa pamoja naye wakamsuta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ati yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke kutoka msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu Kristo, mfalme wa Waisiraeli, ashuke sasa hivi msalabani, tuvione, tupate kumtegemea! Hata wale waliowambwa misalabani pamoja naye wakamtukana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Hata wale waliosulibiwa pamoja naye wakamfyolea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kristo, Mufalme wa Waisraeli, ajishushe sasa juu ya musalaba, kusudi nasi tupate kuona na kumwamini.” Hata wale waliotundikwa pamoja naye walimutukana vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Nao waliosulibiwa pamoja nae wakamlaumu,