Mark 15:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu mmoja akakimbia, akaichovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuone kama Elia atakuja kumteremsha msalabani!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Isa ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Ilya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu mmoja alikimbia na kujaza sifongo kwenye siki, akaliweka kwenye ufito, na akampa Yesu anywe akisema, “Subiri! Tuone ikiwa Eliya atashuka na kumshusha chini.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu mmoja akakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu mmoja akakimbia, akaichovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuone kama Elia atakuja kumteremsha msalabani!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi, akampa Yesu ili anywe akisema, “Basi mwacheni, hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Isa ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Ilya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumteremsha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu mmoja akakimbia, akaichovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuone kama Elia atakuja kumteremsha msalabani!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmoja akapiga mbio, akachovya mwani sikini, akautia katika utete, akamnywesha akisema: Acheni, tuone, kama Elia anakuja kumshusha!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mumoja wao akaenda mbio, akachovya kikausho ndani ya divai yenye kuchacha na kukifungia juu ya tete. Kisha akakipandishia Yesu, kusudi apate kunywa, akisema: “Mwache tuone kama Elia atakuja kumushusha juu ya musalaba.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu akapiga mbio, akajaza sifongo siki, akaitia jim ya unyasi, akamnywesha, akisema, Acheni; na tuone kwamba Eliya anakuja kumshusha.