Mark 15:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria Magdalene, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Palikuwa na wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali. Miongoni mwao walikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya wanawake walikuwa wakiangalia mambo haya toka mbali. Miongoni mwao alikuwapo Maria Magdalena, Salome, na Maria mama yake Yakobo na Yose.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria toka mji wa Magdala, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria Magdalene, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walikuwapo pia wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali, ambao miongoni mwao alikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali. Miongoni mwao walikuwepo Maria Magdalene, na Maria mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwemo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria Magdalene, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Palikuwako nao wanawake, walisimama mbali wakitazama. Kati yao walikuwapo Maria Magadalene na Maria, mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa wanawake wamoja walioangalia kwa mbali. Kati yao kulikuwa Maria wa Magdala, Maria mama ya kijana Yakobo na Yose na mwanamuke mwingine Salome.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; katika hawa alikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama wa Yakobo mdogo na wa Yose, na Salome: