Mark 15:43 — Compare Translations
13 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Arimathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila woga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yusufu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na alikuwa anautarajia ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yusufu wa Arimathea alifika. Yeye alikuwa mjumbe wa Baraza la Kiyahudi aliyeheshimiwa, ambaye pia alikuwa anautazamia ufalme wa Mungu unaokuja. Kwa ujasiri mkubwa aliingia kwa Pilato na kuuomba mwili wa Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Arimathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila woga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yosefu wa Arimathaya mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, ambaye yeye mwenyewe alikuwa anautarajia Ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba huo mwili wa Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yusufu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na ambaye alikuwa anautarajia Ufalme wa Mwenyezi Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Arimathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila woga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akaja Yosefu wa Arimatia aliyekuwa mkuu mwenye macheo; naye mwenyewe alikuwa akiungoja ufalme wa Mungu. Akajipa moyo, akaingia kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akaenda Yusuf, mtii wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza la mashauri, nae mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.