Mark 15:45 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu kuuchukua mwili wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yusufu ruhusa ya kuuchukua huo mwili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule akida, alimpa Yusufu yule maiti.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliposikia taarifa kutoka kwa yule afisa wa jeshi, ndipo alipoutoa mwili wa Yesu na kumpa Yusufu wa Arimathea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu kuuchukua mwili wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yosefu ruhusa ya kuuchukua huo mwili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yusufu ruhusa ya kuuchukua huo mwili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata alipokwisha kupata hakika kutoka kwa yule kamanda, alimpa Yusufu yule maiti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu kuuchukua mwili wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipotambulishwa na bwana askari akampa Yosefu mwili wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule akida, alimpa Yusufu yule maiti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokwisha kuhakikishwa na yule mukubwa wa waaskari kwamba Yesu amekwisha kufa, akamuruhusu Yosefu atwae maiti yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta alipokwisha kupata hakika, akamtunukia Yusuf maiti.