Mark 15:46 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Yusufu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili kutoka msalabani, akaufunga katika kile kitambaa cha kitani, na kuuweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akanunua sanda ya kitani, akamtelemsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Yusufu alinunua mavazi kadhaa ya hariri, na akamshusha Yesu toka msalabani, akauzungushia mwili wake na hariri hiyo, na kumweka katika kaburi lililokuwa limechongwa katika mwamba. Kisha alivingirisha jiwe kubwa na kuliweka mlangoni mwa kaburi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Yosefu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili wa Yesu kutoka msalabani, akauviringishia kile kitambaa cha kitani na akamweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akalivingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Yusufu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili kutoka msalabani, akaufunga katika kile kitambaa cha kitani, na kuuweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akanunua sanda ya kitani, akamteremsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akanunua sanda, akamshusha msalabani, akamtia katika ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani, akafingirisha jiwe mlangoni pa kaburi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akanunua sanda ya kitani, akamtelemsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yosefu akanunua vitambaa, akaondoa maiti ya Yesu juu ya musalaba, akaifungafunga na vile vitambaa na kuiweka ndani ya kaburi lililochimbwa ndani ya jiwe. Kisha wakasukumia jiwe kwenye kiingilio cha lile kaburi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akanunua saanda, akamshusha, akamfungia ile saanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani: akafingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.