Mark 15:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo, mtu aliyeitwa Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na waasi wengine waliokuwa wametekeleza uuaji wakati wa maasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Palikuwa na mtu aitwaye Baraba, amefungwa pamoja na watu waliofanya fitina, na kufanya uuaji katika fitina ile.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu mmoja aliyeitwa Baraba alikuwa gerezani amefungwa pamoja na waasi. Watu hawa walifanya mauaji wakati wa fujo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo, mtu mmoja aitwaye Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na waasi wengine waliokuwa wamesababisha mauaji wakati wa maasi yaliyotokea dhidi ya serikali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo, mtu aliyeitwa Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na waasi wengine waliokuwa wametekeleza uuaji wakati wa maasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Palikuwa na mtu aitwaye Baraba, aliyefungwa pamoja na waasi, waliosababisha mauaji katika uhalifu huo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwako mtu, jina lake Baraba, alifungwa pamoja na watu waliofunga kondo na kuua watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Palikuwa na mtu aitwaye Baraba, amefungwa pamoja na watu waliofanya fitina, na kufanya uuaji katika fitina ile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa mufungwa mumoja, jina lake Baraba, aliyefungwa pamoja na waasi wamoja kwa sababu ya uuaji na uasi walioufanya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Palikuwa na mtu aitwae Barabba, amefungwa pamoja na watu waliofanya fitina na kufanya uuaji katika fitina.