Mark 16:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mariamu akaenda, naye akawaambia wale waliokuwa wamefuatana na Isa, waliokuwa wanaomboleza na kulia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya Mariamu kumwona Yesu, alienda na kuwaeleza wanafunzi wake. Walikuwa wamehuzunishwa sana na walikuwa wakilia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maria akaenda akawaambia wale waliokuwa wakifuatana na Yesu, ambao walikuwa wanaomboleza na kulia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maria akaenda, naye akawaambia wale waliokuwa wamefuatana na Isa, waliokuwa wanaomboleza na kulia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao walikuwa wanaomboleza na kulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipokwenda, akawasimulia wale waliokuwa pamoja naye, walipoomboleza na kulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyu akaenda kupasha habari kwa wale waliokuwa wakikaa pamoja na Yesu. Walikuwa wakiomboleza na kulia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Huyu akashika njia akawapa khabari wale waliokuwa pamoja nae tangu zamani, wangali wakiomboleza na kulia.