Mark 16:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwa ishara zilizoandamana nao. ]
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wanafunzi wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana Isa akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo.]
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na mitume wakatoka na kwenda kuhubiri kila mahali, na Bwana alifanya kazi pamoja nao akithibitisha kuwa ujumbe wao ni wa kweli kwa ishara zilizofuatana na mahubiri yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwa ishara zilizoandamana nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwa ishara zilizoandamana nao.]
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wanafunzi wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wanafunzi wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana Isa akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo.]
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwa ishara zilizoandamana nao. ]
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wale wakatoka, wakapiga mbiu mahali po pote. Naye Bwana alifanya kazi pamoja nao akilitia Neno lake nguvu na kutenda vielekezo vilivyowafuata.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wanafunzi wakaenda kuhubiri fasi zote. Bwana akatumika pamoja nao na kuhakikisha ukweli wa mahubiri yao kwa njia ya vitambulisho walivyofanya.]
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao wakatoka, wakakhubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithubutishia neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Amin.