Mark 16:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakatoka pale kaburini mbio, maana walitetemeka kwa hofu na kushangaa. Hawakumwambia mtu yeyote kitu, kwa sababu waliogopa mno. [
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wakatoka, wakakimbia kutoka mle kaburini wakiwa na hofu kuu na mshangao. Nao hawakumwambia mtu yeyote neno lolote, kwa sababu waliogopa. [
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingia tetemeko na ushangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa. [
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo wale wanawake walitoka na kukimbia kutoka kaburini, kwa sababu hofu na mshangao ulikuwa umewajia. Nao hawakusema chochote kwa mtu yeyote kwani waliogopa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakatoka pale kaburini mbio, maana walitetemeka kwa hofu na kushangaa. Hawakumwambia mtu yeyote kitu, kwa sababu waliogopa mno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakatoka pale kaburini mbio, maana walitetemeka kwa hofu na kushangaa. Hawakumwambia mtu yeyote kitu, kwa sababu waliogopa mno. [
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wakatoka wakakimbia kutoka mle kaburini, kwani hofu kuu na mshangao ulikuwa umewapata, nao hawakumwambia mtu ye yote neno lo lote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wakatoka, wakakimbia kutoka mle kaburini wakiwa na hofu kuu na mshangao. Nao hawakumwambia mtu yeyote neno lolote, kwa sababu waliogopa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingiwa na hofu na mshangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa. [
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakatoka pale kaburini mbio, maana walitetemeka kwa hofu na kushangaa. Hawakumwambia mtu yeyote kitu, kwa sababu waliogopa mno. [
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakatoka kaburini, wakakimbia, kwani walikuwa wameshikwa na utetemeko na ushangao. Kisha hawakumwambia mtu neno, kwani waliogopa.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingia tetemeko na ushangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa. [
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi walitoka kwenye kaburi na kukimbia mbio. Walikuwa wakitetemeka na kushangaa sana. Nao hawakumwambia mutu yeyote, kwa sababu waliogopa. [
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakatoka humo, wakakimbia kutoka kaburini: kwa maana waliingia tetemeko na ushangao: wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.