Mark 2:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipokuwa akipita, akamwona Lawi mwana wa Alfayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate!” Lawi akasimama, akamfuata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa akitembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru. Isa akamwambia, “Nifuate.” Naye Lawi akaondoka, akamfuata Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alipokuwa akitembea kando ya ufukwe wa ziwa, alimwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi katika mahala pake pa kukusanyia kodi. Yesu akamwambia, “Nifuate!” Hivyo Lawi akainuka na kumfuata.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipokuwa akipita, akamwona Lawi mwana wa Alfayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate!” Lawi akasimama, akamfuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipokuwa akipita, akamwona Lawi mwana wa Alfayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate!” Lawi akasimama, akamfuata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokuwa akitembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi forodhani mahali pa kukusanya kodi, akamwambia, “Nifuate.” Lawi akaondoka, akamfuata Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa akitembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru, akamwambia, “Nifuate.” Lawi akaondoka, akamfuata Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipokuwa akipita, akamwona Lawi mwana wa Alfayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate!” Lawi akasimama, akamfuata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha alipokuwa akitembea akamwona Lawi, mwana wa Alfeo, amekaa forodhani. Akamwambia: Nifuata! Akainuka, akamfuata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha alipokuwa akipita, akamwona Lawi mwana wa Alfayo, akiikaa katika nyumba ya kulipishia kodi. Yesu akamwambia: “Unifuate!” Naye Lawi akasimama na kumufuata.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta alipokuwa akipita akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.