Mark 2:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, baadhi ya waalimu wa sheria ambao walikuwa Mafarisayo walipomwona Yesu akila pamoja na watu wenye dhambi na watozaushuru, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini anakula pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walimu wa Torati waliokuwa Mafarisayo walipomwona akila pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, wakawauliza wanafunzi wake: “Mbona Isa anakula na watoza ushuru na wenye dhambi?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa pamoja na Mafarisayo walipomwona Yesu akila na wenye dhambi na wanaokusanya kodi, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini Yesu anakula na wenye kukusanya kodi na watu wengine wenye dhambi?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, baadhi ya walimu wa Sheria ambao walikuwa Mafarisayo walipomwona Yesu akila pamoja na watu wenye dhambi na watoza ushuru, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, baadhi ya waalimu wa sheria ambao walikuwa Mafarisayo walipomwona Yesu akila pamoja na watu wenye dhambi na watozaushuru, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini anakula pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya walimu wa sheria na Mafarisayo walipomwona akila pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, wakawauliza wanafunzi wake, “Mbona Yesu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya walimu wa Torati waliokuwa Mafarisayo walipomwona akila pamoja na watoza ushuru na “wenye dhambi,” wakawauliza wanafunzi wake: “Mbona Isa anakula pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, baadhi ya waalimu wa sheria ambao walikuwa Mafarisayo walipomwona Yesu akila pamoja na watu wenye dhambi na watozaushuru, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini anakula pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waandishi wa Kifariseo walipomwona, ya kuwa anakula pamoja na wakosaji na watoza kodi, wakawaambia wanafunzi wake; Kumbe anakula pamoja na watoza kodi na wakosaji!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wakati walimu wa Sheria wa kikundi cha Wafarisayo walipomwona Yesu akikula pamoja na watu wale, wakawauliza wanafunzi wake: “Kwa sababu gani anakula pamoja na walipishaji wa kodi na watenda mabaya?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Kwa nini anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?