Mark 2:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi wanafunzi wa Yahya pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Watu wakamjia Isa na kumuuliza, “Mbona wanafunzi wa Yahya na wa Mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku moja wafuasi wa Yohana Mbatizaji na Mafarisayo walikuwa wanafunga. Baadhi ya watu walimjia Yesu na kumwuliza, “Mbona wafuasi wa Yohana na wafuasi wa Mafarisayo wanafunga, lakini kwa nini wanafunzi wako hawafungi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wanafunzi wa Yohana pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Baadhi ya watu wakamjia Yesu na kumwuliza, “Mbona wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wanafunzi wa Yahya pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Baadhi ya watu wakamjia Isa na kumuuliza, “Mbona wanafunzi wa Yahya na wa Mafarisayo hufunga lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanafunzi wa Yohana na Mafariseo walikuwa wakifunga. Wakaja, wakamwambia: Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafariseo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wa Yoane Mubatizaji na Wafarisayo walikuwa wakifunga kula chakula. Hivi watu wakakuja kumwuliza Yesu: “Sababu gani wanafunzi wa Yoane Mubatizaji na wanafunzi wa Wafarisayo wanafunga kula chakula, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wanafunzi wake Yohana nao wa Mafarisayo walikuwa wakifunga: wakaja, wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wra Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?