Mark 2:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akajibu, “Je, walioalikwa harusini hutakiwa kufunga wakati bwana arusi yupo pamoja nao? Wakati wote wawapo pamoja na bwana arusi hawawezi kufunga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kufunga wakati angali pamoja nao? Wakati bwana arusi bado yuko pamoja nao, hawawezi kufunga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawajibu, “Katika sherehe ya arusi hutarajii marafiki wa bwana arusi wawe na huzuni wakati yeye mwenyewe yupo pamoja nao. Hakika hawatafunga ikiwa bwana arusi bado yuko pamoja nao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akajibu, “Walioalikwa harusini wanawezaje kufunga kama bwana harusi yupo pamoja nao? Wakati wote wawapo pamoja na bwana harusi hawawezi kufunga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akajibu, “Je, walioalikwa harusini hutakiwa kufunga wakati bwana arusi yupo pamoja nao? Wakati wote wawapo pamoja na bwana arusi hawawezi kufunga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kufunga wakati bwana arusi akiwa pamoja nao? Maadamu bwana arusi yuko pamoja nao, hawawezi kufunga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kufunga wakati angali pamoja nao? Wakati bwana arusi bado yuko pamoja nao, hawawezi kufunga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akawaambia, Walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana harusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana harusi pamoja nao hawawezi kufunga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akajibu, “Je, walioalikwa harusini hutakiwa kufunga wakati bwana arusi yupo pamoja nao? Wakati wote wawapo pamoja na bwana arusi hawawezi kufunga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akawaambia: Walioalikwa arusini hawawezi kufunga, bwana arusi akingali pamoja nao. Siku zote, wanapokuwa na bwana arusi, hawawezi kufunga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawajibu: “Munafikiri kwamba wanaoalikwa kwa arusi wanaweza kujizuiza kula chakula cha karamu wakati bwana-arusi angali pamoja nao? Hapana! Wakati bwana-arusi angali pamoja nao hawawezi kujizuiza kula.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akawaambia, Wana wa arusi wawezaje kufunga maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? Maadam Bwana arusi yupo pamoja nao hawawezi kufunga.